Umoja wa Mataifa

 • flag of the united nations.svg

  umoja wa mataifa (um) ni umoja wa nchi zote duniani isipokuwa zile zisizotambuliwa kuwa dola huru.

  umoja huo ulianzishwa na nchi washindi wa vita kuu ya pili ya dunia kuchukua nafasi ya shirikisho la mataifa (1919 - 1946). makubaliano yalifikiwa tarehe 24 oktoba 1945 huko san francisco, california.

  mwanzoni nchi zilikuwa 51 lakini kufikia mwaka 2017 kulikuwa na nchi wanachama 193, mbali ya ukulu mtakatifu (vatikani) na palestina ambazo zinashiriki kama watazamaji wa kudumu, zikiwa na haki karibu zote isipokuwa kupiga kura.

  dhumuni la umoja huu ni kuratibu mahusiano ya kimataifa kupitia sheria na mikataba ya kimataifa kwenye maeneo kama usalama, amani, maendeleo ya jamii na ya uchumi, haki za binadamu, uhuru, demokrasia n.k.

  toka mwanzo makao makuu ya umoja wa mataifa yako manhattan, new york city, new york nchini marekani na hayako chini ya mamlaka ya nchi hiyo. ofisi nyingine ziko geneva (uswisi), nairobi (kenya) na vienna (austria).

  lugha rasmi za um ni sita: kiarabu, kichina, kifaransa, kihispania, kiingereza na kirusi.

  katibu mkuu wa um anachaguliwa kwa miaka mitano; kwa sasa ni antónio guterres kutoka ureno, aliyechaguliwa kuwa katibu mkuu mwaka 2016 akichukua nafasi ya ban ki-moon.

 • muundo wa um
 • vyama vya pekee vya um
 • viungo vya nje

Flag of the United Nations.svg

Umoja wa Mataifa (UM) ni umoja wa nchi zote duniani isipokuwa zile zisizotambuliwa kuwa dola huru.

Umoja huo ulianzishwa na nchi washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kuchukua nafasi ya Shirikisho la Mataifa (1919 - 1946). Makubaliano yalifikiwa tarehe 24 Oktoba 1945 huko San Francisco, California.

Mwanzoni nchi zilikuwa 51 lakini kufikia mwaka 2017 kulikuwa na nchi wanachama 193, mbali ya Ukulu mtakatifu (Vatikani) na Palestina ambazo zinashiriki kama watazamaji wa kudumu, zikiwa na haki karibu zote isipokuwa kupiga kura.

Dhumuni la umoja huu ni kuratibu mahusiano ya kimataifa kupitia sheria na mikataba ya kimataifa kwenye maeneo kama usalama, amani, maendeleo ya jamii na ya uchumi, haki za binadamu, uhuru, demokrasia n.k.

Toka mwanzo makao makuu ya Umoja wa Mataifa yako Manhattan, New York City, New York nchini Marekani na hayako chini ya mamlaka ya nchi hiyo. Ofisi nyingine ziko Geneva (Uswisi), Nairobi (Kenya) na Vienna (Austria).

Lugha rasmi za UM ni sita: Kiarabu, Kichina, Kifaransa, Kihispania, Kiingereza na Kirusi.

Katibu Mkuu wa UM anachaguliwa kwa miaka mitano; kwa sasa ni António Guterres kutoka Ureno, aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mwaka 2016 akichukua nafasi ya Ban Ki-moon.

Other Languages
Afrikaans: Verenigde Nasies
Alemannisch: Vereinte Nationen
অসমীয়া: ৰাষ্ট্ৰসংঘ
Boarisch: UNO
Bikol Central: Nagkakasararong Nasyon
беларуская (тарашкевіца)‎: Арганізацыя Аб’яднаных Нацыяў
বাংলা: জাতিসংঘ
বিষ্ণুপ্রিয়া মণিপুরী: জাতিসংঘ
Mìng-dĕ̤ng-ngṳ̄: Lièng-hăk-guók
dolnoserbski: Zjadnośone narody
estremeñu: Nacionis Unías
Nordfriisk: Feriand Natjuunen
贛語: 聯合國
Avañe'ẽ: Tetãnguéra Joaju
गोंयची कोंकणी / Gõychi Konknni: संयुक्त राश्ट्रसंघटना
客家語/Hak-kâ-ngî: Lièn-ha̍p-koet
Fiji Hindi: United Nations
hornjoserbsce: Zjednoćene narody
Kreyòl ayisyen: ONI
Bahasa Indonesia: Perserikatan Bangsa-Bangsa
日本語: 国際連合
la .lojban.: gunma natmi
Kabɩyɛ: ONU ŋgbɛyɛ
kalaallisut: FN
한국어: 유엔
kernowek: Kenedhlow Unys
Lëtzebuergesch: Vereent Natiounen
Lingua Franca Nova: Nasiones Unida
македонски: Обединети нации
ဘာသာ မန်: ကုလသမဂ္ဂ
မြန်မာဘာသာ: ကုလသမဂ္ဂ
Plattdüütsch: Vereente Natschonen
Nederlands: Verenigde Naties
norsk nynorsk: Dei sameinte nasjonane
ߒߞߏ: ߡ.ߟ.ߛ
Papiamentu: Nashonan Uni
پنجابی: اقوام متحدہ
armãneashti: Natsiile Unite
ᱥᱟᱱᱛᱟᱲᱤ: ᱡᱟᱹᱛᱤ ᱜᱟᱫᱮᱞ
sardu: ONU
sicilianu: Nazzioni Uniti
davvisámegiella: Ovttastuvvan našuvnnat
srpskohrvatski / српскохрватски: Ujedinjene nacije
Simple English: United Nations
Gagana Samoa: Malo Aufaatasi
Soomaaliga: Qaramada Midoobay
Seeltersk: Fereende Natione
oʻzbekcha/ўзбекча: Birlashgan millatlar tashkiloti
vèneto: ONU
Tiếng Việt: Liên Hiệp Quốc
吴语: 联合国
Vahcuengh: Lenzhozgoz
中文: 联合国
文言: 聯合國
Bân-lâm-gú: Liân-ha̍p-kok
粵語: 聯合國