Televisheni
English: Television

TV ya Kijerumani ya mwaka wa 1956.

Televisheni (kifupi: TV) au runinga ni chombo (kifaa) chenye kiwambo (kioo) ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti.

Neno "televisheni" linatokana na maneno mawili: tele (kutoka Kigiriki: kwa mbali sana) na visio (kutoka Kilatini: mwono; kwa pamoja yanaunda neno la Kiingereza television lililotoholewa katika Kiswahili televisheni.

Historia ya televisheni

TV Braun HF 1 ya Kijerumani ya mwaka wa 1959.

Kwa kawaida TV inaonekana kama sanduku. TV za zamani kabisa zilikuwa zina kirimba au fremu kubwa ya mbao na zilikuwa zikiwekwa chini kama fanicha. TV za kisasa ziko za namna nyingi kama zilivyo nyingi zaidi. Kuna baadhi ya TV zinaweza kuenea mkononi mwako zikawa zinaendeshwa kwa kutumia betri. TV nyingine zinaweza kuenea ukuta mzima wa nyumba, na inaweza kukaa katika sakafu, au kuna nyingine ambazo zimenyooka (flat) na zinaweza kubandikwa ukutani.

Televisheni inaweza kuonyesha picha kutoka sehemu mbalimbali. Cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kutumia kidaka mawasiliano au antena (au aerial), hii itaonyesha yale yote yanayorushwa na kituo cha matangazo ya televisheni.

Vituo vya TV vinaweza kuwa mbali kabisa lakini bado matangazo yake yanapatikana kama antena ya kurusha mawimbi yake iko katika umbali wa kilomita 50 hadi 150. Teknolojia mpya zaidi ni kutumia vyombo vya angani kama antena ya kurusha mawimbi haya duniani. TV pia inaweza kuonyesha filamu kutoka VCD na DVD au VCR yaani tepu za kawaida. Cable TV na Satellite TV zinaweza zikatoa huduma nyingi za vipindi vya TV kwa mara moja na vilevile kuvirusha hewani. Michezo mingi ya video huunganishwa katika TV ili uweze kuona kile unachokicheza. Kuna baadhi ya tarakilishi au kompyuta ambazo unaweza kutumia TV kama kioo cha kufanyia kazi zako (kiwambo, au kwa jina lingine monita). TV za kisasa ( TV janja, kwa Kiingereza: Smart TV) zina uwezo wa kutumia intaneti moja kwa moja.

TV zote zina kiwambo ambacho kinaonyesha picha. Kabla ya miaka ya 1970 TV zilikuwa hazina rangi (yaani zilikuwa "black and white" tu), ambazo zilikuwa zinafanya kila kitu kionekane cha rangi ya kijivu. Lakini kwa sasa karibuni TV zote zinaonyesha na rangi. Kawaida ya viwambo vingi (kioo au vioo) huonyesha kuwa vina kona ya mzunguko, lakini kwa sasa vioo vingi hutengenzwa kwa kunyooka na zina ncha pembeni.

Njia ya picha katika TV

Kabla ya miaka ya 1990, TV zote zilikuwa zikitengenezwa kwa umbo moja - zilikuwa kubwa kidogo na kisha zilikuwa ndefu. Kwa mfano, kama kioo kilikuwa cha urefu wa inchi 3, basi lazima kitakuwa na upana wa inchi 4. Au kama kioo kina urefu wa cm 30, lazima kitakuwa kina upana wa cm 40.

Umbo la TV za kisasa linazidi kuwa maarufu na kupata wapenzi wengi zaidi kila siku ziendapo. TV zenye kioo cha upana mkubwa wa mstatili huonekana vizuri katika runinga kubwa (theatre screen) na pia inapendeza wengi zaidi. Hizi huziita kioo kipana (widescreen). Endapo TV ya kioo kipana ina urefu wa cm 30, basi lazima itakuwa ina upana wa cm 53. Ili ifanye kazi vizuri, uonyeshaji wa TV pia unatakiwa ujengwe kwa namna ya upana yaani 'widescreen'. Kioo kipana kinaweza kubadilishika kwa ukubwa wowote unaoutaka, lakini suala la umbo linabaki kuwa vilevile kama lilivyo (widescreen).

Other Languages
Afrikaans: Televisie
Alemannisch: Fernsehen
አማርኛ: ቴሌቪዥን
aragonés: Televisión
Ænglisc: Feorrsīen
العربية: تلفاز
ܐܪܡܝܐ: ܦܪܣ ܚܙܘܐ
অসমীয়া: দূৰদৰ্শন
asturianu: Televisión
azərbaycanca: Televiziya
تۆرکجه: تلویزیون
башҡортса: Телевидение
žemaitėška: Televėzėjė
беларуская: Тэлебачанне
беларуская (тарашкевіца)‎: Тэлебачаньне
български: Телевизия
भोजपुरी: टेलीविजन
বাংলা: টেলিভিশন
brezhoneg: Skinwel
bosanski: Televizija
буряад: Телевиз
català: Televisió
Mìng-dĕ̤ng-ngṳ̄: Diêng-sê
qırımtatarca: Telekörüv
čeština: Televize
kaszëbsczi: Telewizjô
Чӑвашла: Телекурăм
Cymraeg: Teledu
dansk: Fjernsyn
Deutsch: Fernsehen
Thuɔŋjäŋ: Atoockïït
Zazaki: Têlevizyon
Ελληνικά: Τηλεόραση
emiliàn e rumagnòl: Televisiån
English: Television
Esperanto: Televido
español: Televisión
euskara: Telebista
estremeñu: Televisión
فارسی: تلویزیون
suomi: Televisio
Na Vosa Vakaviti: Television
føroyskt: Sjónvarp
français: Télévision
arpetan: Tèlèvision
Frysk: Telefyzje
Gaeilge: Teilifís
贛語: 電視
Gàidhlig: Telebhisean
galego: Televisión
Avañe'ẽ: Ta'ãngambyry
गोंयची कोंकणी / Gõychi Konknni: दूरचित्रवाणी
Bahasa Hulontalo: Televisi
Hausa: Talabijin
客家語/Hak-kâ-ngî: Thien-sṳ
Hawaiʻi: Kelewikiona
עברית: טלוויזיה
हिन्दी: दूरदर्शन
Fiji Hindi: Television
hrvatski: Televizija
Kreyòl ayisyen: Televizyon
magyar: Televízió
interlingua: Television
Bahasa Indonesia: Televisi
Iñupiak: Taġġiraun
Ilokano: Telebision
íslenska: Sjónvarp
italiano: Televisione
日本語: テレビ
Patois: Telivijan
ქართული: ტელევიზია
Taqbaylit: Tiliẓri
Kabɩyɛ: Televiziyɔɔ
Gĩkũyũ: Terebiceni
қазақша: Телевидение
ភាសាខ្មែរ: ទូរទស្សន៍
ಕನ್ನಡ: ದೂರದರ್ಶನ
한국어: 텔레비전
कॉशुर / کٲشُر: ٹٮ۪لِوِجَن
kurdî: Televîzyon
Кыргызча: Телекөрсөтүү
Latina: Televisio
Ladino: Televizyón
Lëtzebuergesch: Televisioun
Lingua Franca Nova: Televisa
Limburgs: Tillevies
Ligure: Televixon
lumbaart: Television
lietuvių: Televizija
latviešu: Televīzija
मैथिली: टेलिभिजन
Basa Banyumasan: Televisi
Malagasy: Televiziona
македонски: Телевизија
മലയാളം: ടെലിവിഷൻ
монгол: Телевиз
Bahasa Melayu: Televisyen
Mirandés: Telbison
မြန်မာဘာသာ: တယ်လီဗစ်ရှင်း
مازِرونی: تیلوزیون
Plattdüütsch: Feernseher
Nedersaksies: Televisy
नेपाली: टेलिभिजन
नेपाल भाषा: टेलेभिजन
Nederlands: Televisie
norsk nynorsk: Fjernsyn
norsk: Fjernsyn
Novial: Televisione
Nouormand: Télévision
occitan: Television
ਪੰਜਾਬੀ: ਟੈਲੀਵਿਜ਼ਨ
Papiamentu: Television
Picard: Télévision
Deitsch: Guckbax
polski: Telewizja
پنجابی: ٹیلیوژن
پښتو: تلويزون
português: Televisão
Runa Simi: Ñawikaruy
română: Televiziune
русский: Телевидение
русиньскый: Телевізія
संस्कृतम्: दूरदर्शनम्
саха тыла: Телевидение
ᱥᱟᱱᱛᱟᱲᱤ: ᱧᱮᱱᱮᱞᱚᱢ
sicilianu: Televisioni
srpskohrvatski / српскохрватски: Televizija
slovenčina: Televízia (prenos)
slovenščina: Televizija
Gagana Samoa: Televise
Soomaaliga: Telefishin
српски / srpski: Телевизија
Seeltersk: Fiersjoon
Basa Sunda: Televisi
svenska: Television
ślůnski: Telewizyjo
తెలుగు: టెలివిజన్
тоҷикӣ: Телевизион
ትግርኛ: ቲቪ
Türkmençe: Telewizor
Tagalog: Telebisyon
Türkçe: Televizyon
татарча/tatarça: Телевидение
ئۇيغۇرچە / Uyghurche: تېلېۋىزور
українська: Телебачення
oʻzbekcha/ўзбекча: Televideniya
vèneto: Tełevixion
Tiếng Việt: Truyền hình
walon: Televuzion
Winaray: Telebisyon
吴语: 电视机
მარგალური: ტელევიზია
ייִדיש: טעלעוויזיע
Yorùbá: Tẹlifísàn
Zeêuws: Tillevisie
中文: 电视
文言: 電視
Bân-lâm-gú: Tiān-sī
粵語: 電視