Okavango

Mto wa Okavango
Feri juu ya mto Okavango nchini Botswana
ChanzoNyanda za juu za Bié (Angola)
MdomoDelta ya barani katika jangwa la Kalahari, Botswana
NchiAngola, Namibia, Botswana
Urefu1,600 km
Kimo cha chanzo1,780 m
Mkondo10,000,000,000 m³/mwaka (inaweza kukauka kwa muda)
Eneo la beseni721.258 km²
Delta ya Ovango inavyoonekana kutoka angani

Okavango (pia: Okovango; katika Angola: Kubango au Cubango) ni mto wa Afrika ya kusini-magharibi. Inaanza nchini Angola katika milima ya Bié inapojulikana kwa jina la Kubango. Mwendo wake wa 1600 km ni kusini tu hadi jangwa la Kalahari inapoishia kwenye delta ya barani. Katika kusini ya Angola ni mpaka na Namibia. Inapita nchi ya Namibia mwanzoni wa kishoroba ya Caprivi na kuendelea Botswana inapoishia jangwani katika delta yake.

Jina la mto limepatikana kutoka kabila la Wakavango.

Chanzo cha mto ni kusini ya mji wa Vila Nova (Angola) katika milima ya Bié kwenye kimo cha 1,780 m. Mwanzoni mwendo wake ni ya haraka kuna maporomoko madogo. Halafu mto ni mpaka kati ya Angola na Namibia. Baada ya kupokea tawimto wa Kwito inaingia Namibia inapopita kanda nyembamba ya kishoroba ya Caprivi kwa kilomita chache. Kabla ya kuvuka mpaka wa Botswana mto unashuka mita 4 kwenye maporomoko ya Popa.

Takriban 70 km ndani ya Botswana mwendo wa mto unapanuka na kugawanyika kuwa delta ya barani yenye zaidi ya 16,000 km².

Other Languages
Afrikaans: Okavangorivier
azərbaycanca: Okavanqo çayı
беларуская: Акаванга
беларуская (тарашкевіца)‎: Акаванга (рака)
български: Окаванго
brezhoneg: Okavango
bosanski: Okavango
català: Okavango
čeština: Okavango
Cymraeg: Afon Okavango
Deutsch: Okavango
Esperanto: Okavango
español: Okavango
eesti: Okavango
euskara: Okavango
français: Okavango
hrvatski: Okavango
magyar: Okavango
հայերեն: Օկավանգո
Bahasa Indonesia: Sungai Okavango
íslenska: Okavangofljót
italiano: Okavango
한국어: 오카방고강
lietuvių: Okavangas
македонски: Окаванго
Nederlands: Okavango
norsk: Okavango
occitan: Okavango
português: Rio Cubango
română: Okavango
саха тыла: Окаванго
srpskohrvatski / српскохрватски: Okavango
slovenčina: Okavango
slovenščina: Okavango
српски / srpski: Окаванго
svenska: Okavango
Türkçe: Okavango Nehri
українська: Окаванґо