Manga
English: Manga

Herufi ya lugha ya Kijapani kutoka kitabu Seasonal Passersby (Shiki no Yukikai), 1798, kilichotungwa na Santō Kyōden na Kitao Shigemasa.

Manga (ja: 漫画 kanji: まんが katakana: マンガ English: /ˈmɑːŋɡə/) ni hadithi zinazotungwa kwa kutumia michoro (wakati mwingine pia hujulikana kama komikku katika lugha ya Kijapani. Hufuata jinsi ya kuchora ulioendelezwa Ujapani mwishoni mwa karne ya 20. Katika namna zake za kisasa, manga zilianza muda mfupi baada ya Vita vikuu vya pili [1], lakini aina hii ya sanaa ina historia ndefu katika miaka awali ya sanaa ya Ujapani.

Katika Ujapani, watu wa umri wote husoma manga. Manga ni aina ya sanaa inayojumuisha mapana ya mada kama vile: "action-adventure", mapenzi (kWa Kiingereza romance), michezo (sports and games), drama za kihistoria (historicsl dramas), vichekesho (comedy), hadithi ya chuku yanayohusu sayansi (science fiction), fumbo (mystery), hadithi ya kutisha (horror), ngono (sexuality), na biashara (business and commerce), miongoni mwa nyingine. [2]

Tangu miaka ya 1950, manga imekua na kujiendeleza hadi sasa inawakilisha sehemu kubwa ya sekta ya kuchapisha humo Ujapani, ni sekta iliyowakilisha yen bilioni 406 katika soko nchini Japan mnamo mwaka 2007 (wastani wa dola bilioni 3.6). Manga imekuwa maarufu duniani kote pia. [3] Mwaka wa 2008, soko la manga katika nchi za Marekani na Kanada ilikuwa $ milioni 175.

Manga kwa kawaida huchapishwa bila rangi, yaani huwa nyeusi-na-nyeupe, ingawa kuna baadhi ya manga zinazochapishwa kutumia rangi zote. Katika Ujapani, manga kawaida huchapishwa katika vitabu vyenye kurasa nyingi, huenda vitabu hivi huhusisha hadithi tofauti, na kila hadithi huendelezwa katika suala la kufuata. Mfululizo ukiwa na mafanikio, sura zilizokusanywa zinaweza kuchapishwa tena katika vitabu viitwayo tankōbon. [4] Msanii wa manga (mangaka kwa Kijapani) kawaida hufanya kazi na wasaidizi wachache katika studio ndogo na pamoja na mhariri kutoka kampuni ya kuchapisha. [1] Manga ikiwa maarufu inaweza kubadilishwa kuwa kipindi kinachoweza kutazamwa katika runinga baada au hata wakati ambako inachapishwa, [5] Wakati mwingine manga zinazohusisha filamu zilizopo awali hutunzwa (k.m. Star Wars).

Neno "Manga" hutumika nje ya Ujapani kumaanisha vitabu vya michoro viliyochapishwa nchini Ujapani. [6] Hata hivyo, vitabu vya michoro vilivyoshawishiwa kutoka manga vipo katika maeneo mengine ya dunia, hasa katika Taiwan (manhua), Korea ya Kusini (manhwa) [7] na Jamhuri ya Watu wa China, hasa Hong Kong (manhua). [8] Katika Ufaransa, la Nouvelle manga ina maendeleo kama aina ya bande dessinée (yaani drawn strip) inayotolewa katika mitindo iliyoshawishiwa na manga kutoka Ujapani. Katika Marekani, watu hurejelea vitabu vinavyofanana na manga kama Amerimanga, manga ya dunia, au manga yenye asili ya lugha ya Kiingereza ("original english language manga" - OEL manga).

Other Languages
Afrikaans: Manga
Alemannisch: Manga
አማርኛ: ማንጋ
aragonés: Manga
العربية: مانغا
مصرى: مانجا
asturianu: Manga
azərbaycanca: Manqa
беларуская: Манга (мастацтва)
беларуская (тарашкевіца)‎: Манга
български: Манга
Bahasa Banjar: Manga
বাংলা: মাঙ্গা
བོད་ཡིག: མན་གྷ།
বিষ্ণুপ্রিয়া মণিপুরী: মাঙ্গা
bosanski: Manga
català: Manga
čeština: Manga
Cymraeg: Manga
dansk: Manga
Deutsch: Manga
Ελληνικά: Manga
English: Manga
Esperanto: Mangao
español: Manga
eesti: Manga
euskara: Manga
فارسی: مانگا
suomi: Manga
français: Manga
Gaeilge: Manga
贛語: 漫畫
galego: Manga
Gaelg: Manga
עברית: מאנגה
हिन्दी: मांगा
hrvatski: Manga
magyar: Manga
հայերեն: Մանգա
Bahasa Indonesia: Manga
íslenska: Manga
italiano: Manga
日本語: 日本の漫画
Basa Jawa: Manga
ქართული: მანგა
қазақша: Манга
ಕನ್ನಡ: ಮಂಗಾ
한국어: 일본 만화
kurdî: Manga
Кыргызча: Манга
Latina: Manga
Lëtzebuergesch: Manga
lumbaart: Manga
lietuvių: Manga
latviešu: Manga
македонски: Манга
монгол: Манга
Bahasa Melayu: Manga
Nāhuatl: Manga
Napulitano: Manga
Nederlands: Manga (strip)
norsk: Manga
ଓଡ଼ିଆ: ମାଂଗା
ਪੰਜਾਬੀ: ਮਾਂਗਾ
polski: Manga
português: Mangá
Runa Simi: Manga
română: Manga
русский: Манга
sardu: Manga
Scots: Manga
davvisámegiella: Manga
srpskohrvatski / српскохрватски: Manga
Simple English: Manga
slovenčina: Manga
slovenščina: Manga
shqip: Manga
српски / srpski: Manga
Basa Sunda: Manga
svenska: Manga
ślůnski: Manga
தமிழ்: மங்கா
ไทย: มังงะ
Tagalog: Manga
українська: Манґа
اردو: مانگا
oʻzbekcha/ўзбекча: Manga
Tiếng Việt: Manga
Winaray: Manga
吴语: 日本漫画
Yorùbá: Mángà
中文: 日本漫画
Bân-lâm-gú: Ji̍t-pún bàng-gah
粵語: 日本漫畫