Kamera
English: Camera

Kamera
Kamera.

Kamera ni kifaa kinachochukua picha. Ina tundu moja dogo tu kwa kupokea nuru inayoacha picha ndani yake ama kwenye filamu au kwenye kihisio elektroniki. Kwa kawaida nafasi hii huwa na lenzi inayozalisha picha ya yale yaliyo nje.

Kamera tuli hushika picha moja-moja. Picha zinazopigwa mfululizo, angalau picha 15 kwa sekunde au zaidi, zinaweza kushika mwendo utakaoonekana baadaye kama filamu kama picha hizi zinaonyeshwa mfululizo kwa kutumia projekta au kwenye skrini ya sinema runinga au kompyuta.

Kamera zote kimsingi ni sanduku inayofungwa pande zote. Nuru haiwezi kuingia mpaka kilango kinafunguliwa n kupitisha nuru kwa kipindi kifupi cha sehemu ya sekunde pekee. Kilango hiki kipo nyuma ya lenzi. Kwa upande mwingine ni wenzo maalum ambao unaweza kurekodi picha ambayo inakuja kupitia lenzi. Wenzo huu ni filamu katika kamera ya filamu au kihisio elektroniki katika kamera dijiti.

Wakati picha inachukuliwa, kilango kinatoka nje ya njia. Hii inawezesha nuru kuingia kwa njia ya lenzi na kuzalisha picha kwenye filamu au kihisio elektroniki. Katika kamera nyingi, ukubwa wa tundu unaweza kubadilishwa kulingana na mwangaza au giza ya mazingira. Muda ambao kifuniko kinauwezesha mwanga inaweza pia kubadilishwa. Hii pia inakuwezesha mwanga zaidi au mwanga mdogo. Mara nyingi, umeme ndani ya kamera hudhibiti haya, lakini katika kamera nyingine mtu anayeichukua picha anaweza kubadilisha pia.

Lenzi humwezesha mpigapicha kuvuta mbali au karibu picha anayoipiga. Kwa njia hii mpigapicha anapata uwezo wa kupiga kwa urahisi picha ya kitu kilicho mbali au kitu kidogo sana na kupata picha safi.

Kamera nyingi huwa na lenzi yake na uwezo wa kuongezewa lenzi nyingine ya nje kulingana na kazi inayolengwa kufanywa. Lenzi za nje zina uwezo na urefu wa kuona tofauti kulingana na ukubwa wake na idadi ya lenzi zinazotumika. Kuna lenzi za nje za kamera za simu pia.

Tanbihi

Other Languages
Afrikaans: Kamera
Ænglisc: Sīensearu
العربية: كاميرا
Boarisch: Kamera
भोजपुरी: कैमरा
বাংলা: ক্যামেরা
བོད་ཡིག: པར་ཆས།
bosanski: Kamera
català: Càmera
Mìng-dĕ̤ng-ngṳ̄: Kiák-sióng-gĭ
کوردی: کامێرا
Cymraeg: Camera
dansk: Kamera
Deutsch: Kamera
Zazaki: Kamera
English: Camera
Esperanto: Fotilo
euskara: Kamera
فارسی: دوربین
suomi: Kamera
français: Caméra
Frysk: Kamera
Gaeilge: Ceamara
贛語: 相機
客家語/Hak-kâ-ngî: Hip-siông-kî
עברית: מצלמה
हिन्दी: कैमरा
Bahasa Indonesia: Kamera
Ido: Kamero
íslenska: Myndavél
日本語: カメラ
Patois: Kiamara
Jawa: Kodhak
ភាសាខ្មែរ: កាមេរ៉ា
ಕನ್ನಡ: ಕ್ಯಾಮರ
한국어: 사진기
कॉशुर / کٲشُر: کیمرا
kurdî: Wênekêş
Lingua Franca Nova: Camera
Limburgs: Camera
latviešu: Kamera (ierīce)
Malagasy: Fakan-tsary
македонски: Камера
മലയാളം: ഛായാഗ്രാഹി
मराठी: कॅमेरा
Bahasa Melayu: Kamera
မြန်မာဘာသာ: ကင်မရာ
नेपाली: क्यामरा
Nederlands: Camera
norsk: Kamera
Sesotho sa Leboa: Khamêra
ଓଡ଼ିଆ: କ୍ୟାମେରା
ਪੰਜਾਬੀ: ਕੈਮਰਾ
پښتو: انځورۍ
português: Câmera
Runa Simi: Rikch'a hap'ina
संस्कृतम्: छायाग्राहिका
ᱥᱟᱱᱛᱟᱲᱤ: ᱠᱮᱢᱨᱟ
Scots: Camera
සිංහල: කැමරව
Simple English: Camera
Soomaaliga: Sawirqaado
српски / srpski: Камера
Basa Sunda: Kaméra
svenska: Kamera
తెలుగు: కెమెరా
Tagalog: Kamera
українська: Знімальна камера
اردو: کیمرا
Tiếng Việt: Máy ảnh
Winaray: Kamera
მარგალური: ფოტოაპარატი
ייִדיש: קאמערע
中文: 照相機
Bân-lâm-gú: Hip-siòng-ki
粵語: 相機